Monday, March 12, 2012

Van Persie akubali offer ya Man City?

Manchester City wako tayari kumfanya Robin Van Persie kuwa mchezaji anayelipwa mshara mkubwa kuliko mchezaji yoyote kwenye ligi kuu ya Uingereza, ambapo atakua akipokea kiasi cha paundi 210,000 kwa wiki.

Mkataba huo unathamani ya paundi milioni 10.9 kwa mwaka, Chazo kimoja cha The Sunday Times kimeripoti kwamba kimsingi Van Persie amekubali dili hilo litalomuingizia kitita kikubwa cha pesa.

Bado timu zote mbili za Manchester City na Arsenal hazijafanya makubaliano rasmi, Ingawa Arsenal inaonekana kutaka kumzuia mshambuliaji huyo nyota aliyepiga mabao 32 katika michezo 37 aliyocheza msimu huu asiondoke klabuni hapo.

Van Persie 28 anatarajia kumaliza mkataba wake na Arsenal mwisho wa msimu ujao (mwezi wa sita 2013) na kocha wa Manchester city amekua akielezea ni kwa kiasi gani anamkubali mshambulijai huyo.

Mario Balotelli na Yaya Toure nusura wazichape kavukavu

Wachezaji wa Manchester City Mario Balotelli na Yaya Toure nusura wazichape kavukavu wakati timu zinaenda mapumziko kwenye mechi dhidi ya Swansea City kwenye mfululizo wa mechi za ligi kuu ya Uingereza hapo jana, Mechi hiyo iliisha kwa Manchester City kulala kwa bao moja bila majibu.

Chombo cha habari cha The Sun kilieleza kuwa utata huo ulizuka baada ya wachezaji hao wawili kuanza kurushiana maneno kwa sauti kali wakati wakielekea kwenye vyumba vya kubadilishia nguo.Iliwachukua muda kidogo wachezaji hao kurejea dimbani kuendelea na mchezo huo wakati kipindi cha pili kilipoanza.

Wakati wanaelekea kwenye vyumba vya kubadilishia nguo Balotelli na Toure walionekana wakitetea jambo fulani kwa umakini wa hali ya juu. Lakini mambo yalibadilika walipoingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo na wakasikika wakikaripiana kwa hasira. Ingawa kocha wao Roberto Mancini alisema hajui lolote kuhusiana na suala hilo.

Alipoulizwa, kocha huyo raia wa Italia alisema “Hapana, sijui lolote kusiana na suala hilo.”

Suarez ajipendekeza mwenyewe PSG

Klabu ya Liverpool ya Uingereza imeshtushwa na taarifa za mshambuliaji wao wa Kutegemewa Luis Suarez kutamani kucheza pamoja na mchezaji mwenzake wa Urguay Diego Lugano anayekipiga kunako klabu ya PSG.

Suarez aliuambia mtandao wa 10 Sport kwamba “Ningependa kucheza klabu moja nae (Lugano). Ndio naweza kuja Paris.Kuna klabu nyingi zenye pesa ambazo zina

Manchester United kileleni

Wayne Rooney ameiweka Manchester United kileleni kwenye msimamo wa ligi kwa tofauti ya pointi moja baada ya kushinda mchezo wao wa Ligi Kuu ya Uingereza dhidi ya West Bromwich Albion 2-0 katika uwanja wa Old Trafford, matokeo ambayo yamepokewa kwa furaha zaidi na mashabiki wa United hasa baada ya mahasimu wao wakubwa na waliokuwa wakiongoza ligi, Manchester City kukubali kipigo cha 1-0 nyumbani kwa Swansea City.

Kwa matokeo hayo, United wamefikisha jumla ya pointi 67 huku City akibaki na pointi zake 66.

Mchezo mwingine ambao umeanza hivi punde unazikutanisha Norwich City wanaoikaribisha Wigan Athletic.

2011-2012 LIGI KUU YA BARCLAYS

Kwa ujumla
Nyumbani
Ugenini

Nafasi
Timu P W D L F A
W D L F A
W D L F A
GD Pts
1 Manchester United 28 21 4 3 68 27
11 1 2 39 15
10 3 1 29 12
41 67
2 Manchester City 28 21 3 4 69 20
14 0 0 42 6
7 3 4 27 14
49 66
3 Tottenham Hotspur 28 16 5 7 52 34
10 2 2 30 13
6 3 5 22 21
18 53
4 Arsenal 27 15 4 8 55 38
9 2 2 29 11
6 2 6 26 27
17 49


Saturday, March 10, 2012

Roberto Mancini amkasirisha Wenger

Kocha wa Arsenal Arsene Wenger amekasirishwa na kitendo cha Kocha wa Manchester City Roberto Mancini Kuongea hadharani kuelezea jinsi anavyomujhitaji Van Persie kwenye timu yake.

Gazeti la Uingereza London Evening Standard limesema kwamba Wenger amepatwa na hasira Kwa kitendo cha Mancini kumuongelea Mchezaji ambaye ana Mkataba na Timu mpaka mwaka 2013,Kwa sasa wenger Anapata wakati mgumu kuhakikisha Van Persie anaingia Mkataba mpya na Arsenal.

Van Persie Ameomba makubaliano juu Mkataba mpya yasogezwe mbele mpaka Mwisho wa msimu,Na inasemekana kumaliza Ndani ya nne bora kwenye ligi ya Uingereza ndicho kigezo kikubwa kitakachomfanya Van Persie Kubaki Arsenal.

Friday, March 9, 2012

van Persie amtia hofu Wenger

TIMU ya Arsenal imeingia katika hofu kubwa kutokana na hali ilivyo kwa mchezaji wake tegemeo, Robin van Persie ambaye juzi alishindwa kufanya mazoezi na timu yake ya taifa ya Uholanzi, kwa kile kilichoelezwa kusumbuliwa na maumivu.

Mchezaji huyo alishindwa kucheza katika dakika zote pale Uholanzi ilipocheza na England, hivyo kuanza kuwatia hofu mashabiki wa timu hiyo.

Kocha Arsene Wenger amesema kwamba, atafuatilia kwa karibu zaidi afya ya mchezaji huyo.

Drogba ataka mawe zaid chelsea

MSHAMBULIAJI wa Chelsea, Didier Drogba kwa sasa anataka mamilioni ya fedha kwa ajili ya kubaki ndani ya timu hiyo, akitaka apewe kiasi cha pauni milioni 6 kwa mwaka, ikiwa ni baada ya makato ya kodi.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast, kwa sasa amebakiza miezi mitano kabla ya kumaliza rasmi mkataba wake ndani ya timu hiyo na sasa anataka apewe fedha za uhakika.

Drogba ametaka alipwe fedha hizo, ambazo zitakuwa ni mshahara kamili baada ya kuondolewa makato yote

Man City yavutiwa na Van Persie



Kocha wa Manchester City muitalia Roberto Mancini amekiri kuwa anatamani sana kumsajiri kinara wa kupachika mabao wa Arsenal mholanzi Robin Van Persie.

Kuna uvumi kuwa mpachika mabao huyo anaweza akaondoka msimu ujao hasa kutokana na hali ya Arsenal katika kufukuzia taji la Ligi kuu kuwa ndogo na ukame wa vikombe kwa zaidi ya miaka mitano sasa.

Hata hivyo sio rahisi Manchester City ikamchukua kirahisi kwani timu nyingi kubwa za Ulaya zitakuwa nyuma ya ununuzi huo tayari kuvunja akaunti zao mara tuu Arsenal itakapotangaza kumuuza.

Hata hivyo Mancini hana uhakika kama Van Persie ataondoka Arsenal

"Ni mchezaji mzuri sana, lakini nafikiri atabaki na Arsenal. Nafikiri kama kuna mchezaji mzuri atataka kuondoka kwenye klabu yake basi lazima tuvutiwe naye. Lakini kama mchezaji huyu atataka kubaki hatutakuwa na tatizo naye. Kwa maoni yangu, Van Persie atabaki Arsenal" alisema Mancini.

Man U apata Kichapo nyumbani


Mashabiki wa Manchester United walibaki jana vinywa wazi pale timu yao ilipochapwa mabao matatu kwa mbili na Athletico Bilbao katika uwanja wao wa Old Trafford.

Aibu ya kuchapwa nyumbani na Athletico Bilbao

Timu hiyo ya Uhispania iliizidi maarifa mashetani wekundu katika mchuano wa hatua ya timu 16 bora ya mechi za kombe la ligi ya Euro.

Man U ndio waliokuwa wakwanza kufunga bao katika dakika ya 22 kupitia mwamba wake Wayne Rooney. Lakini baada ya hapo Athletico ilianza kuihangaisha ngome ya Manchester United . Na kukiwa kumesalia dakika chache tu kwa timu hizo kwenda mapumziko Fernando Llorente aliisawazishia Athletico Bilbao. Baadae Oscar de Marcos na Iker Muniain wakafanya magoli kuwa 1-3.

Lakini kabla ya kipyenga cha mwisho Rooney aliipatia Man U bao lake la pili kupitia mkwaju wa penalti.

Baada ya mechi hiyo Meneja wa Manchester United akiri kuwa timu yake ilizidiwa maarifa na Athletico Bilbao ya Uhispania.

" Walikuwa wazuri kutushinda . Kwetu itakuwa ni kazi ya kupanda mlima", Ferguson alisema.

Lakini mkufunzi huyo wa Man U bado ni mwingi wa matumaini kwamba wanauwezo wa kifunga Athletico Bilbao watakapowatembelea kwao baada ya wiki mbili.

Man City yanyolewa Ureno.

Itailazimu timu ya Manchester City kujikakamua na kuifunga Sporting Lisbin ya Ureno wiki mbili zijazo baada ya kuchapwa 1-0 ugenini.

Sporting Lisbon washerehekea kwa kuichuna Man City

Hii ilikuwa ni katika mechi za timu 16 bora katika kinyang'anyiro cha kombe la Euro.

Man City walitoka uwanjani wakiwa wanyonge baada ya kuchezewa na vijana wa Ureno ambao walikuwa wakionana vizuri.

Bao la kwanza na la pekee la Sporting lilifungwa na mara tu baada ya kipindi cha lala salama kuanza.

Wadadisi wa soka wanadai kuwa licha yakufungwa huko ,bado Man City inanafasi nzuri ya kuifunga Sporting Lisbon na hatimae kusonga mbele katika michuano hiyo ya kombe la Europa

Bendtner ahofia angekuwa kipofu

Nicklas Bendtner alihofia upofu

Mshambuliaji wa Sunderland Nicklas Bendtner, amesema alikuwa na wasiwasi huenda amepoteza uwezo wa kuona alipoumia jicho katika mechi dhdi ya Swansea City mwezi wa Januari.

Nicklas Bendtner alihofia upofu

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Denmark alipelekwa hospitali baada ya mfupa juu ya jicho lake kuvunjika alipokumbana na mlinzi wa Swansea Angel Rangel.

"Nafurahi kwamba sikupofuka," Bendtner aliiambia BBC.

"Sikuweza kulitumia jicho langu kwa saa nne au tano na pia nililazimika kulazwa hospitalini usiku kucha."

Bendtner, anayechezea Sunderaland kwa mkopo akiwa mchezaji wa Arsenal hadi mwishoni mwa msimu, alifunga bao la kuongoza wakati timu yake ilipotoka sare ya 1-1 dhidi ya Newcastle United siku ya Jumapili.

Mbali ya kurejea katika mechi dhidi ya West Bromwich Albion wiki moja kabla, mshambuliaji huyo hakucheza kandanda kwa muda wa mwezi mmoja alipokuwa akijiuguza na katika mechi mbili zilizopita alikuwa amevaa kifaa maalum cha kukinga uso.

Alisema "Sijali kugongwa au kuvunjika pua ama taya ambayo yatapona tu, lakini macho yako ni muhimu zaidi".

"Mara tu nilipogongwa, sikuweza kuona kitu chochote na mawazo yaliyonijia awali nimepofuka', kwa hiyo nilifarijika kupita kiasi, kwa kutumia mikono yangu, niliweza kufunua jicho na kuona vitu vingi vyekundu.

"Natumai kuna malaika anayelinda.

Podolski kujiunga na Gunners

Klabu ya Arsenal imeafikiana na mshambuliaji wa Ujerumani Lukas Podolski kutoka klabu ya Cologne, BBC Michezo imefahamu.

Kwa mujibu wa taarifa Arsenal italipa pauni za Uingereza £10.9m kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 kwa mkataba wa miaka minne akilipwa pauni £100,000 kila wiki.

Hata hivyo itabidi Podolski amalize utaratibu wa afya yake na kukubaliana juu ya maslahi yake kabla kuhamia London majira ya joto mwaka huu.

Beki wa Arsenal Per Mertesacker amesema kua: "amekua akiwasiliana nami mara kwa mara na nilimfahamisha kuhusu vifaa na kwamba ni mahali pazuri kufanyia kazi na klabu ya Arsenal ni nzuri sana.

Wachezaji hao wamecheza pamoja katika Timu ya Taifa ya Ujerumani tangu mwaka 2004 na wanatazamia kushirikiana katika klabu moja.

Meneja wa klabu ya Cologne Stale Solbakken alikiri mwezi uliopita kua huenda akampoteza mshambuliaji wake huyo Podolski kwa Arsenal na kuongezea kua shughuli za kumsajili zimefikia hatua pevu.

Thursday, March 8, 2012

Teknolojia kwa shule za msingi Zanzibar


MRADI wa Elimu wa Karne ya 21, unaohusiana na elimu ya teknolojia ya habari na mawasiliano kwa shule za msingi, umetajwa kuwa chachu ya maendeleo katika ulimwengu wa utandawazi.

Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein aliyasema hayo jana katika uzinduzi wa mradi huo na kuongeza kuwa watoto wa darasa la kwanza hadi la nne watakuwa wakitumia kompyuta.

Alisema Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ina umuhimu kwa ulimwengu wa sasa na hasa kwa watoto katika kukuza elimu yao ambapo hatua hiyo itawasaidia katika ugunduzi wa maarifa mapya katika masomo, kuchemsha bongo, kurahisisha ufanyaji wa kazi zao na kuokoa muda.

Dk. Shein pia alisisitiza kuwa mabadiliko ya kielimu yanategemea mchango wa walimu wenye kubadilika kitaaluma na katika mbinu za ufundishaji na kueleza kuwa lazima walimu wajifunze kutumia vifaa vya kisasa yakiwemo matumizi ya kompyuta.

Dk. Shein alisema Serikali itaendelea kuwatengenezea mazingira bora walimu ili wazidi kupata moyo katika kutekeleza majukumu yao na kutoa wito kwa walimu kuendelea kuchapa kazi.

Dk. Shein alipongeza uamuzi wa Serikali ya Marekani kwa kupitia Shirika lake la Maendeleo (USAID) kwa kutoa msaada huo unaogharimu dola za marekani milioni 50 ambao utakuwa wa miaka mitano.

Naye Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Alfonso Lenhardt alisema mradi huo ni msingi muhimu wa kuleta mabadiliko makubwa ya teknolojia ya habari na mawasiliano Zanzibar.

Aidha, Balozi Lenhardt alisema kuwa elimu ina umuhimu kwa vijana wa Tanzania kwani ndio silaha katika maisha yao na kusisitiza kuwa mradi huo utakapomalizika unatarajiwa kuwanufaisha zaidi ya walimu 4,094, shule za msingi na sekta za elimu.

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Zahra Ali Hamad alisema mradi huo utaweza kuwasaidia walimu na wanafunzi kupata taaluma ya teknolojia ya habari na kuzidisha uimarishaji wa sekta ya elimu nchini.

Awali Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, Mwanaidi Saleh alieleza kuwa mbali ya kushughulikia utoaji wa elimu kwa walimu na wanafunzi, mradi huo pia unahusika na kuweka utaratibu mzuri wa kukusanya taarifa na takwimu ya masuala ya elimu.

Alisema kuwa Mradi wa matumizi ya teknolojia ya kisasa katika elimu utahusisha shule 248 za msingi, kati ya hizo shule 45 zitapatiwa vifaa zaidi kwa mujibu wa sifa zilizowekwa ambapo majaribio ya mradi yameanza katika shule ya Kisiwandui na Daraji na Kituo cha Walimu Michakaeni.

Alisema kuwa vituo vyote 10 vya walimu vitapatiwa vifaa vya kisasa ili viweze kutoa mafunzo kwa walimu kwa ufanisi zaidi.

King Messi aweka rikodi ulaya ( UEFA )


Magoli matano kutoka kwa Mchezaji bora wa dunia kwa mara mbili mfululizo raia wa Argentina, Lionel Messi katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, hatua ya 16 bora yameweka rekodi mpya kwa mchezaji mmoja kufunga idadi ya mabao hayo katika mechi moja kwenye mashindano ya ngazi ya vilabu yanayoandaliwa na chama cha soka barani Ulaya (UEFA).

Ikicheza nyumbani, Camp Nou, mbele ya mashabiki wake Barcelona iliitandika bila ya huruma Bayer Leverkusen 7 – 1. Ushindi mkubwa waliowahi kupata Barcelona katika uwanja wa nyumbani kwenye mashindano ya ngazi ya UEFA.

Messi alipatia Barcelona magoli kunako dakika za 24, 42, 49, 58 na 84 huku kinda Cristian Tello akitupia nyavuni magoli mawili katika dakika za 62 na 65 katika mechi yake ya kwanza katika mashindano ya UEFA.

Leverkusen walipata bao la kufutia machozi kupitia kwa Karim Bellarabi katika dakika za nyongeza.

Baada ya ushindi wa 3 – 1 katika mechi ya kwanza nyumbani kwa Leverkusen, Barcelona imesonga kwenye hatua ya robo fainali kwa jumla ya mabao 10 – 2.

Katika mechi nyingine APOEL Nicosia iliitandika Lyon 1 – 0 na kufanya matokeo ya jumla kuwa 1 – 1 baada ya wao kufungwa la Lyon 1 – 0 katika mchezo wa kwanza. Hata hivyo Nicosia walisonga katika robo fainali baada ya kushinda kwa mikwaju ya penati.

Gonzalo Higuain kuhamia Juventus


Higuain kwenda Juventus

Mshambuliaji wa Real Madrid Gonzalo Higuain anaweza kuhamia Juventus, habari kutoka kwa baba yake mzazi. Tovuti ya ESPN soccernet imeripoti.

Higuain ambaye ana miaka 24, amekuwa akihusishwa na kuondoka Bernabeu, ingawa mkataba wake sasa unaisha mwaka 2016, na Paris St Germain wamekiri kuwa watamuhitaji mchezaji huyo katika majira ya joto.

Hata hivyo JJuventus wamekuwa na mahusiano toka zamani na Jorge Higuain, babake Gonzalo na wakala wake., wamejihakikishia uwezekano wa kwenda Turin upo.

‘Ni faraja kuvutiwa na Juventus’ aliimbia Tuttosport. “Kwa sasa, Higuain anafikiria zaidi kuhusu Madrid, lakini mwezi mei tutaweza zungumza”

Juventus pia inasemekana wamevutiwa na kijana wa miaka 17 kutoka River Plate, Lucas Ocampos, ambae mkataba wake unaisha 2013

Wakala Pablo Martin Sabbag aliimbia Calcio Mercato: “naweza kukuhakikishia timu nyingi kutoka ulaya wanavutiowa nae”

Alipoulizwa kuhusu Juventus akaongeza, “Sipendelei kutaja majina, lakini naweza kusema timu tatu kutoka Italia zinamfuatilia”

Lucas Podolski ndani ya the Gunners


Arsenal Yakamilisha Uhamisho wa Lucas Podolski

Mshambuliaji wa Ujerumani Lucas Podolski atakua mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Arsenal wakati dirisha la usajili litakapofunguliwa baada ya Arsenal kukubaliana na Cologne(Klabu ya zamani ya Podolski) kwa kiasi cha paundi 10.9 milioni.

Hapo awali Cologne walikua wanahitaji kiasi cha paundi 18 milioni ambacho kilikataliwa na Arsenal ambao walikua tayari kutoa kiasi cha paundi 8 milioni.Arsenal walianza kufanya makubaliano binafsi na Podolski(26) kabla ya kuweka offer mpya iliyokubaliwa na Cologne.

Lucas Podolski mzaliwa wa Poland mwenye miaka 26 ameshafunga magoli 16 katika michezo 20 aliyochezea Cologne katika ligi ya Bundesliga(Ujerumani) msimu huu.

Lucas Podolski alisajiliwa na Cologne akitokea Bayern Munich mwaka 2009.Akiwa Bayern Munich Podolski hakufanikiwa kufanya vizuri hivyo kumfanya kukaa benchi kwenye mechi nyingi.Hata hivyo Podolski amekua na mafanikio mazuri kwenye timu ya Taifa ya Ujerumani akifanikiwa kufunga magoli 43 hivyo kumfanya kuwa mchezaji wa sita wa Ujerumani kuwahi kufunga magoli mengi kwenye ngazi ya taifa.

Wednesday, March 7, 2012

Maafisa wa polisi wauwa Pakistan

Watu waliojihami kwa bunduki na maguruneti wamewauwa maafisa watatu wa polisi katika mji wa Peshawar Kaskazini Magharibi mwa Pakistan.

Watu watatu walishambulia kituo cha polisi katikati mwa mji huo na kisha kujilipua pale polisi walipoanza kuwakabili.
Ripoti zaidi zinasema polisi wengine wanne walijeruhiwa.

Wanamgambo wamekuwa wakiulenga mji wa Peshawar mara kwa mara katika miaka ya hivi karibuni.

Eneo hilo ni ngome ya wanamgambo walio na uhusiano na makundi ya Taliban na Al-Qaeda.

Benghazi yajitangazia utawala wake


Viongozi wa wapiganaji na wa makabila katika mji wa Benghazi nchini Libya wamejitangazia utawala wao katika eneo la mashariki mwa nchi kama jimbo lenye uhuru.

Wanasema wanarejea makubaliano ya tangu miaka ya 1950 ya jimbo hilo, likijulikana kama Cyrenaica, lilivyoendeshwa kwa asilimia kubwa ya utawala.

Wengi wa watu wa Benghazi wamekuwa wakilalamika kuachwa nyuma na kubaguliwa kwa jimbo lao ambalo lina utajiri mkubwa wa mafuta Hatua hiyo inaleta wasiwasi kwa utawala wa muda mjini Tripoli.

Mwandshi wa BBC Gabriel Gatehouse aliyeko mjini Benghazi katika sherehe hizo amlisema mamia ya watu walikusanyika katika eneo la kuegeshea ndege katika kitongoji kimoja cha jiji la Benghazi.

Walicheza ngoma huku wakitoa kauli za kuunga mkono mfumo wa shirikisho.

Msemaji wa Baraza la wananchi wa Cyrenica aliiambia BBC kwamba makabila na wanajeshi wanaliunga mkono azimio linalohimiza eneo la Mashariki ya Libya lijitawale wenyewe.

Cyrenaica ina utajiri mkubwa wa mafuta na hatua hii itachochea taharuki ya ugomvi katika Tripoli na kwingineko kuwania udhibiti wa mali asili za Libya.

Lakini watu wake wanasema wanachokitaka ni kugawana sawasawa utajiri huo.

Azimio lao halina mashiko ya kisheria .

Kwa sasa Libya iko katika hali ya taharuki za kisiasa lakini baada ya miongo kadhaa ya kutengwa,hatua hii inaungwa mkono na wengi katika mji huu wa pili kwa ukubwa nchini Libya.

Somalia yataka afrika mashariki


Somalia ambayo imekua ikijaribu kujikwamua toka vita vya miaka 20 imetuma maombi yakutaka kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Kenya ambayo ndio mwenyekiti wa sasa wa Jumuiya hiyo imethibitisha kupokea maombi ya Somalia.

Taarifa kutoka serikali ya mpito ya Somalia inasema kuwa wameamua kujiunga na jumuiya hiyo kutokana na hali ya kiusalama nchini Somalia kuimarika na utulivu kuanza kushuhudiwa.

Somalia inakuwa nchi ya tatu baada ya Sudan Kusini na Sudan Khartoum kutuma maombi ya kutaka kujiunga na Jumuiya hiyo ya Afrika Mashariki.

Hata hivyo azma ya Sudan kutaka kujiunga na jumuiya hiyo ya Afrika Mashariki imekataliwa.

Kwa sasa jumuiya ya Afrika Mashariki inajumuisha nchi tano, Kenya, Tanzania, Uganda, Rwanda na Burundi.

Mbali na nchi wanachama kuwa na ruhusa ya kufanya biashara bila vikwazo vyovote kwa wakati huu zinapanga kuwa na sarafu moja kufikia mwaka mwezi Juni mwaka huu wa 2012

Tuesday, March 6, 2012

OSCE,"Uchaguzi wa urais Urusi siyo huru"


Uchaguzi wa urais nchini Urusi ulipangwa kuhakikisha Vladmir Putin anapata ushindi. Hii ni kwa mujibu wa waangalizi kutoka shirika huru la Organisation for Security and Co-operation (OSCE).Matokeo ya mapema yameonyesha Waziri Mkuu Putin akiwa na asili mia 63.

OSCE imesema uchaguzi huo ulighubikwa na visa vingi vya udnganyifu na hauwezi kutajwa kuwa huru. Vyama vya upinzani vimeomba kuwepo na maandamano dhidi ya ushindi wa Putin.Taarifa ya shirika hilo imesema japo wagombea waliweza kufanya kampeini zao, masharti na utaratibu wote uliwekwa kuhakikisha Waziri Mkuu Vladimir Putin anatwaa ushindi.

Msemaji wa shirika hilo Tonino Picula ameongeza hakukuwa na ushindani na kampeini za upande wa serikali ziliendeshwa kwa kutumia ralimali za umma. Awali kundi nyingine la waangilizi kutoka Urusi Golos lilisema serikali iliingilia utaratibu wa uchaguzi huku kukiwa na visa vya wapiga kura kulazimishwa kumchagua kiongozi fulani.

Golos imempa Bw. Putin kura chache juu ya asili mia 50 kinyume na matokeo ya tume ya uchaguzi.Hata hivyo katika mkutano wa hadhara, mjini Moscow Bw.Putin alisema alishinda wazi bila udanganyifu.

Vladimir Putin, alirejea wadhifa wa Waziri Mkuu mwaka 2008 baada ya katiba kumzuia kuwania awamu ya tatu mtawalia kama rais. Ushindi wa sasa utamfanya kusalia madarakani hadi 2018 na anachukua nafasi ya Dmitry Medvedev.

Uchaguzi wa urais nchini Urusi umefanyika huku kukiwa na malalamishi ya udanganyifu katika uchaguzi wa ubunge hapo mwezi Decemba mwaka jana.

Vilipuzi vimetapakaa Congo Brazzaville


Bado ni hatari kuingia eneo ambapo milipuko ilitokea siku ya Jumapili katika mji mkuu wa Congo, Brazzaville. Waokoaji wanasema kufikia sasa bado kunamilipuko midogo midogo ambayo ingali inashuhudiwa.

Taarifa zinazohusiana Afrika,ajali

Na mwandishi wa BBC amesema inahofiwa kuwa kuna mamia ya maiti ambazo huenda zingali katika vifusi vya majengo yalioporomoka kutokana na milipuko hiyo ya Jumapili.

Serikali inasema idadi ya waliofariki ni 146 . Hata hivyo takwimu kutoka vyumba vya kuhifadhia maiti na madaktari wanasema kuwa idadi ya waliofariki imefikia zaidi ya 200 na wale waliojeruhiwa ni 1,500

Na maafisa wa kijeshi wamenukuliwa wakisema kuwa hatari nyegine inayokabili watu ni kutapakaa kwa vilipuzi . Hii inaleta hofu kuwa moto huenda ukatokea katika ghala la pili la silaha

Hospitali zilizoko Brazzaville zinawakati mgumu kukabiliana na idadi kubwa ya majeruhi.

Watu waliokuwa wakiishi karibu na kambi ya kijeshi nchini Congo, bado wanaendelea na shughuli ya kujaribu kuokoa mabaki ya mali yao iliyoteketea kufuatia mlipuko uliotokea katika kambi hyo na kusababisha vifo vya zaidi ya watu miaka moja hamsini.

Nyingi ya nyumba zilizokuwa karibu na kambi hiyo ya kijeshi ilikuwa imejengwa kwa mabati. Watu hao wanasema walipoteza mali yao yote wakati wa mlipuko huo uliosababisha na hitilafu za nguvu za umeme katika ghala moja ya silaha.

Ukuta unaozunguka kambi hiyo ya kijeshi ilianguka licha ya kuwa imejengwa na saruji.

Mmoja wa manusura wa mlipuko huo ameiambia BBC kuwa atajaribu kutafuta makaazi kutoka kwa jamaa wake na ikiwa atakosa atalazimika kuishi katika kambi za muda zilizojengwa na serikali.

Amesema miili ya watu ilikuwa imetapakaa katika bara bara za mji huo baada ya mlipuko huo siku ya jumapili.

Misaada ya kibinadamu inaendelea kutolewa kwa manusura wa mkasa huo. Hospitali kuu ya mjini humo bado inapokea watu waliojeruhiwa.

Baadhi yao wanaendelea kupkea matibabu katika hema zilizojengwa nje ya hospitali hiyo ya chuko kikuu na shirika na madaktari wasio na mipaka Médecins sans Frontières

Waziri wa huduma za jamii nchini humo na kamishna mkuu wa muungano wa ulaya kuhusu misaada ya kibinadm wamesema kuwa suala kuu kwa sasa ni kuhakikisha kuwepo kwa madaktari zaidi hasa madaktari wa upasuaji ili kutibu wale waliojeruhiwa.

Tatizo lingine linalokabili serikali ya nchi hiyo ni suala la silaha zilizotawanyika wakati wa mlipuko huo.

Mwakilishi wa shirika moja linalojihusiha na harakati za kupinga utumizi mabomu za kuzikwa ardhini, amesema raia kadhaa walionekana wakikusanya mabomu ya aina hiyo ambao haikulipuka bila kuwa na vifaa vya kujilinda.

Vile vile usalama wa kambai hiyo sio dhabiti kufuatia mkasa huo. Amesema kundi lake lilikuwa limetambua athari za ghala hilo la silaha wakati wa ziara yao katika kambi hiyo na kuwa walifahamisha utawala wa nchi hiyo na hawakuchukua hatua zozote.

Uturuki yaanza safari za ndege Somalia


Shirika la ndege la Uturuki inatarajiwa kuwa shirika la kwanza kuanzisha safari za ndege hadi mjini Mogadisho Somalia.

Ndege ya Uturuki kuwasili Mogadishu

Naibu wa Waziri mkuu wa Uturuki Bekir Bozdag siku ya Jumanne anatarajiwa kusafiri katika ndege hiyo.
Taarifa zinazohusiana

Naibu huyo wa Waziri Mkuu pia amepangiwa kuzindua miradi mbali mbali za maendeleo mjini humo.

Mashirika ya usafiri wa ndege nchini Somalia yamekuwa na safari kati ya Somalia, Djibouti, Kenya na nchi za Kiarabu pekee.

Hii itakuwa safari ya Kwanza kutoka mataifa ya magharibi kuingia Mjini Mogadishu kwa mara ya kwanza tangu mwaka wa1991 na itakuwa na safari mbili kwa wiki kupitia Khartoum.

Nimezungumza na mbunge Hussein Bantu na kwanza nilimuuliza je Uturuki itaweza kweli kuendesha safari kama hii nchini Somalia.

Shirika hilo la Ndege la Uturuki limepanga kufanya safari mbili kila wiki kati ya Istanbul na Mogadishu.

Hatua hii inakuja wakati baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linakutana mjini New York kujadiliana kuhusu Somalia.

Akizungumza na Idhaa ya Kisomali ya BBC waziri wa Uingereza anayehusika na maswala ya Afrika Henry Bellingham alisema jamii ya kimataifa imeamua kuwa huu ndio wakati muafaka wa Somalia kupata amani na uthabiti wa kudumu.

Waziri huyo ambaye kwa niaba ya Uingereza ,ndiye mwenyekiti wa Baraza hilo katika Mwezi huu wa Machi, amesema mkutano huo ulikubali mapendekezo yote yalioafikiwa katika mkutano wa hivi majuzi wa London kuhusu Somalia.

FREEMASONS IN TANZANIA


Kama unadhani kizazi hiki kinachoabudu ibada za Kabballah (wayahudi) na chenye kujiona ni zaidi ya binadamu wengine, kwamba ni kidogo utakuwa unajidanganya. Kama unadhani kizazi hiki kinatoa misaada kwa watoto yatima, na watoto waishio katika mazingira magumu unajidanganya.

Kama unadhani kutembelea tovuti yao yenye kujipambaunua kwamba inasaidi jamii kwa kiasi kikubwa, basi unajilimbikizia ujuha. Kama unadhani Freemasonry wapo Dar es salaam pekee basi uko nyuma yam shale wa saa unavyokwenda.

Iwapo ulidhani huna ndugu ambaye anaajira za Freemasonry basi unaweza kujidanganya pia huku ukijigamba kwamba unazo pesa za ‘kumwaga’. Na kama unadhani kuna mfanyabiashara nchini ambaye anatoa sana misaada kwa jamii kwamba inatokana na mavuno yake, basi unajidanganya.

Kama unaamini hutumii bidhaa za Freemasonry unajiongopea mwenyewe. Ni wakati wako wa kuchunguza kipi kipo wapi na nini kinaendelea nchini mwetu. Ziko pesa, badhaa na mabo lukika yenye nembo za Freemasons ambayo wewe unadhani ni muhimu katika maisha yako. Kifupi wametukamata.

Freemasons wasikudanganye kwamba wao ni imani za mwenyezi mungu ambaye amewatuma kuja kuwasaidia watu wenye dhiki. Kama ni hivyo basi tusingeliona utawala wa Marekani unakuwa wa Ki-Freemasons na kumaliza maisha ya Wairak, Wavietnam na kwingineko.

Na walivyo na sura za upole na kuchukuliwa kama watoa misaada kwa watu masikini, basi tumewapa tiketi ya kuziingilia nyumba zetu watakavyo. Ndiyo ni miaka 79 sasa kizazi hiki cha shetani kinachoruhusu wanaume pekee kuingia humo. Umejiuliza kwanini wanawake hawakubaliki? Tafakari.

Kwa taarifa yako kuna binadamu anaitwa Rockefeller anataka binadamu wote tuwekewe Microchip ili taarifa zetu zichukuliwe na satellite na kuziweka katika kompyuta moja. Wanataka kututawala kimwili sasa baada ya kufanikisha kututawala kiakili.

Rockefeller Mmarekani huyu ni adui namba moja wa binadamu walioumbwa na mwenyezi mungu. Katika azimio hilo ambalo kiambato chake ni New World Order kilichotangazwa n asana muumini wa Freemasons George Bush na ambaye nduguye Marvin Bush alipewa dhamana ya kulinda WTC kabla ya kulishambulia-kisha wakadanganya ni Osama Bin Laden.

Kama unadhani mfumo huu wa Microchip ni dhihaka, nakuachia kiungo hiki msomaji wangu mpendwa umfuatilie kiumbe huyu dhalimu; www.nexusmagazine.com/articles/rockefeller.html. ni kiumbe hatari kama ilivyokuwa kwa Adolf Hitler ambaye alikuwa kiumbe wao.

Ni hawahawa sasa wamejipa mamlaka ya kila kitu katika tawala mbalimbali ikiwemo Tanzania. Na wametushika kwa mambo mengi sana, mara utasiki misaada ya kiutu, mara leo utasikia Vicoba (kuna mkono wa Freemasonry hapo), na mengineyo.

Freemasons wapo nchini Tanzania kwa miaka 79 sasa, wakiendesha shughuli zao na kuwapumbaza watu. Wanafanya hila zao kwa kudai kuwa ni watumishi wa mungu tusiyemuamini. Wanajieleza kwa umakini sana ili kutolipua siri zao.

Soma maneno haya ambayo yalitamkwa na binadamu Sir Jayantilal Kashavji, ‘Once a Freemasons, always a Freemasons’. Inawezekana ikawa mgeni kwako, lakini ukitajiwa binadamu aitwaye Andy Chande siyo geni kwako. Nasadiki kwa dhati kabisa jina la pili limetoakana na kujiunga na Freemasonry.

Tunaambiwa ndani ya miaka 79 kipenzi chetu Mwalimu Nyerere alijua uwepo wao, lakini unaweza kujiuliza swali kwani imesemwa wakati yeye amekwisha kufariki? Na inaelezwa kuwa Mwalimu hakuwa Freemasonry(sijui angelikuwa hai angelisemaje).

Kwa maneno yao wenyewe wanajigamba kwa kusema ‘Freemasons is natural or Instictive fellowship between people of similar interest’. Inawezekana maneno haya yasiwe na maana kwako, lakini kuna swali jepesi moja tu. Je wanawake hawana ‘similar interest’ na Freemasonry (wanaume)?

Maneno yote ninayokupa ndugu msomaji sijatunga, na wala mimi siyo mtungaji wa makala hizi, bali mtafiti. Sitafiti kisha niandike bali nilikwisha kufanya hilo na ninaendelea ndiyo maana nakupa viungo kadhaa ujipe nafasi zaidi.

Mnamo April 3, 2005 Sir Jayantilal Kashavji au Andy Chande alifanya mahojiano na mwandishi mwandamizi Muhidin Michuzi. Msomaji mahojiano hayo yapo katika gazeti la Sunday News la April 3, 2005. Kuna maswali zaidi ya 100 ambayo ninaweza kuyauliza tokana na majibu ya mheshimiwa huyo.

Lakini swali langu la msingi ningelimwuliza kutokana na maneno yake haya; ‘I joined Freemasons 1954. However it took me two years to complete the process’. Kwamba licha ya kujiunga na Freemasons, ilimchukua miaka miwili kumaliza taratibu zote. ‘Taratibu’ zipi hizo iwapo ni jumuiya inayosadiki mungu?

Yaani nikiamua kujiunga na dini mojawapo sasa kati ya Ukristo au Uislamu toka Uafrika wangu, nichukue miaka miwili kumaliza ‘taratibu zote’? Ni taratibu gani mlizopewa enyi kizazi cha nyoka? Kizazi kilichovamia na kufanya mauaji huko Iraq na kuwaua wale wasiokuwa wanachama wao.

Sir Jayantalal Kashavji au J.K Chande au Andy Chande anatanabaisha kuwa kuwa Freemasons ni jumuiya iliyopo chini ya utawala wa United Grand Lodge ya Uingereza na Wales (soma Sunday News la April 3, 2005).

Hakukuwa na jipya sana katika majibu yake kwani inaonekana kulikuwa na ujuvi wa pande mbili kabla na baada ya mahojiano. Tunafahamu kuwa uzinduzi wa Freemasons ulifanyika chini ya utawala wa Rais Benjamini Mkapa, je kuna uhusiano gani kati ya kizazi hicho na uanzishwaji wa Bank M? funua akili yako!

Unaelewa ninachokuuliza na unagundua ninachomaanisha? Kwa maneno yake Andy Chande (Jayantalal Kashavji anawataja viongozi wanaowasapoti; Benjamini Mkapa (Tanzania), Moody Awory (Kenya), na Yoweri Museven (Uganda) kwa eneo la afrika mashariki.

Msomaji ukikumbuka makala mbili zilizopita ninataja sana serikali ya dunia. Na ukitazama uongozi wa J. K Chande unaunganisha Tanzania, Uganda, Shelisheli na Kenya, unaweza kupata jawabu kuwa hili ni jimbo, mtaa, kata ama kijiji cha Freemasons?

Na wengine sasa mnalia kuhusu suala la NICOL, basi unachopaswa kukifahamu kuwa kuna baadhi ya waandamizi wa kizazi cha Freemasonry hapo. Siyo jambo geni na wala halishangazi kwa wanazuoni. Tunajua ni akina nani walihudhuria sherehe ya uzinduzi. Na hata ile ya kutimiza miaka 75 ilipofanyika wakati wa awamu ya tatu.

Kwanini sherehe ya kutimiza miaka 75, mwaka 2005 ilitangazwa kuliko huko nyuma kwamba freemasonry wapo nchini au vinginevyo? Kwani ulikuwa wakati wa kutaja kuwa ni jumuiya isyofahamika kwa watu wakati ni jinsia moja tu inahiutajika?

Unaweza kupuuza sana suala hilo, na kama J.K Chande anavyosema kwa maneno yake mwenyewe haya; ‘Nyerere was not a Freemasons, but he knew what Freemasonry is’. Msomaji unaona ninachokiona hapo? Unaelewa ninachokielewa? Kwamba alifahamu, je ndiye aliyewasajili na kuingia nchini Tanzania?

District Grand Master Jayantalal Kashavji alituhabarisha kuwa ameongoza Freemasons kwa miaka 50 na ameamua kustaafu. Ukitaka kumfahamu bosi mpya wa Freemasons Tanzania nakuachia kiungo hiki; http;//www.ippmedia.com/guardian.2006/10/27/77236.html.

Na kwa wale wasomaji ambao hawana muda wa kutembelea mtandaoni, nakutaka usome gazeti la Guardian la tarehe 27/10/2006 (uk 4) habari iliripotiwa na Judica Tarimo. Hata hivyo wale wanaokubaliana nami, basi wafahamu kuwa bosi huyo ni Suryakant Ramji, msaidizi wake ni Tanna Sreekumar.

Na bosi wa eneo lote la afrika mashariki (yaani Tanzania, Uganda, Kenya na Shelisheli ni Dr Vilendra Talwar). Freemasonry wanawanachama zaidi ya milioni 5 hadi mwaka 2005, kizazi hiki cha nyoka kilianza mwaka karne ya 13. Na kwa Tanzania makao makuu yao ipo mitaa ya Sokoine (Sokoine Drive) mkabala hoteli ya Kilimanjaro jijini Dar es salaam.

Vituko na ibada hizo za kishetani haziko Dar es salaam pekee, huko Arusha zimejazana na historia yake ni inajieleza wazi. Nitaeleza. Mnamo Julai 14, 2001 kulifanyika kikao cha Ki-freemasons Mount Meru Lodge.

Awali makao hayo yalipewa namba ya usajili 5363 kati ya mwaka 1932, lakini uanachama wake ulishamiri zaidi kulipoibuliwa vita ya pili ya dunia. Ndugu msomaji vita hiyo siyo kama tunavyodanganywa katika mashule yetu, kwani wenyewe wanaelewa ninachomaanisha hapa.

Huku vita hivyo vikiendelea, usajili wa ngome mpya za Freemasons ulikuwa ukifanywa. Na Arusha ilikwisha kupata namba ya awali (tazama hapo juu). Hivyo tangu mwaka 1957 Mount Meru Lodge ikapewa namba 7504. Ambapo kikao chao cha awali kilifanyika Kilimanjaro Lodge ya ki-freemasons No. 5111 mjini Moshi.

Kuna wamiliki wa Televisheni, na matajiri wakubwa ambao wanaabudu ibada za kishetani. Wanatumia utajiri huo kuwafumba watu kuwa wao wanasaidia jamii. Wanahadhi kubwa mbele ya watawala wetu, wanaheshimika mbele ya mawakala wa CIA (ambao ni mabalozi tulionao).

Wapo wanaounga mkono u-freemasons Tanzania huku wakiwa wanachama; Dr Edward Tenner (mgunduzi wa Vaccination), Dr William Mayo na Charles Mayo (waanzilishi wa kliniki ya moyo Marekani). Mwanzilishi wa tifa la Uturuki Jenerali Mustafa Kamal Atatuk, Mchungaji William Booth (mwanzilishi wa Salvation Army-jeshi la wokovu).

Wengine Padre Francisco Calvo (Padre wa kikatoliki aliyeanzisha Frremasonry huko Costa Rica mwaka 1865), Mchungaji Jesse Jackson (mwanzilishi wa Rainbow Coalition), Aga Khan (Kiongozi wa madhehebu ya Ismailia) 1877-1957. lakini swali linasalia kuhusu Aga Khan III(je ni mwendelezo wa freemasonry?).

Yupo Thomas Watson! Humfahamu huyu? Unaweza kuitazama kompyuta yako ndugu msomaji, kama imeandikwa IBM huyu ndiye mwanzilishi. Kuna J. Edgar Hoover (mkurugenzi wa FBI). Hapa nikuachie kiungo hiki msomaji; http;//calodges.org/no406.famasons.htm.

Usidanganyike kuwa kizazi hiki kinahubiri dini za mwenyezi mungu unazozijua, na wenyewe wanadai hakuna majadiliano kuhusu dini. Na msomaji aliyeuliza kuhusu Rais Obama, nitamwuliza; je unakumbuka kuwa tuliambiwa kiapo chake cha Urais kilikosewa hivyo wakarudia? Tafakari hilo, nipe jibu.