Tuesday, August 6, 2013
Ligi kuu UK
Ahsante
Monday, March 12, 2012
Van Persie akubali offer ya Man City?
Mkataba huo unathamani ya paundi milioni 10.9 kwa mwaka, Chazo kimoja cha The Sunday Times kimeripoti kwamba kimsingi Van Persie amekubali dili hilo litalomuingizia kitita kikubwa cha pesa.
Bado timu zote mbili za Manchester City na Arsenal hazijafanya makubaliano rasmi, Ingawa Arsenal inaonekana kutaka kumzuia mshambuliaji huyo nyota aliyepiga mabao 32 katika michezo 37 aliyocheza msimu huu asiondoke klabuni hapo.
Van Persie 28 anatarajia kumaliza mkataba wake na Arsenal mwisho wa msimu ujao (mwezi wa sita 2013) na kocha wa Manchester city amekua akielezea ni kwa kiasi gani anamkubali mshambulijai huyo.
Mario Balotelli na Yaya Toure nusura wazichape kavukavu
Chombo cha habari cha The Sun kilieleza kuwa utata huo ulizuka baada ya wachezaji hao wawili kuanza kurushiana maneno kwa sauti kali wakati wakielekea kwenye vyumba vya kubadilishia nguo.Iliwachukua muda kidogo wachezaji hao kurejea dimbani kuendelea na mchezo huo wakati kipindi cha pili kilipoanza.
Wakati wanaelekea kwenye vyumba vya kubadilishia nguo Balotelli na Toure walionekana wakitetea jambo fulani kwa umakini wa hali ya juu. Lakini mambo yalibadilika walipoingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo na wakasikika wakikaripiana kwa hasira. Ingawa kocha wao Roberto Mancini alisema hajui lolote kuhusiana na suala hilo.
Alipoulizwa, kocha huyo raia wa Italia alisema “Hapana, sijui lolote kusiana na suala hilo.”
Suarez ajipendekeza mwenyewe PSG
Suarez aliuambia mtandao wa 10 Sport kwamba “Ningependa kucheza klabu moja nae (Lugano). Ndio naweza kuja Paris.Kuna klabu nyingi zenye pesa ambazo zina
Manchester United kileleni
Kwa matokeo hayo, United wamefikisha jumla ya pointi 67 huku City akibaki na pointi zake 66.
Mchezo mwingine ambao umeanza hivi punde unazikutanisha Norwich City wanaoikaribisha Wigan Athletic.
2011-2012 LIGI KUU YA BARCLAYS | |||||||||||||||||||||||
Kwa ujumla | Nyumbani | Ugenini | |||||||||||||||||||||
Nafasi | Timu | P | W | D | L | F | A | W | D | L | F | A | W | D | L | F | A | GD | Pts | ||||
1 | Manchester United | 28 | 21 | 4 | 3 | 68 | 27 | 11 | 1 | 2 | 39 | 15 | 10 | 3 | 1 | 29 | 12 | 41 | 67 | ||||
2 | Manchester City | 28 | 21 | 3 | 4 | 69 | 20 | 14 | 0 | 0 | 42 | 6 | 7 | 3 | 4 | 27 | 14 | 49 | 66 | ||||
3 | Tottenham Hotspur | 28 | 16 | 5 | 7 | 52 | 34 | 10 | 2 | 2 | 30 | 13 | 6 | 3 | 5 | 22 | 21 | 18 | 53 | ||||
4 | Arsenal | 27 | 15 | 4 | 8 | 55 | 38 | 9 | 2 | 2 | 29 | 11 | 6 | 2 | 6 | 26 | 27 | 17 | 49 |
Saturday, March 10, 2012
Roberto Mancini amkasirisha Wenger
Gazeti la Uingereza London Evening Standard limesema kwamba Wenger amepatwa na hasira Kwa kitendo cha Mancini kumuongelea Mchezaji ambaye ana Mkataba na Timu mpaka mwaka 2013,Kwa sasa wenger Anapata wakati mgumu kuhakikisha Van Persie anaingia Mkataba mpya na Arsenal.
Van Persie Ameomba makubaliano juu Mkataba mpya yasogezwe mbele mpaka Mwisho wa msimu,Na inasemekana kumaliza Ndani ya nne bora kwenye ligi ya Uingereza ndicho kigezo kikubwa kitakachomfanya Van Persie Kubaki Arsenal.
Friday, March 9, 2012
van Persie amtia hofu Wenger
Mchezaji huyo alishindwa kucheza katika dakika zote pale Uholanzi ilipocheza na England, hivyo kuanza kuwatia hofu mashabiki wa timu hiyo.
Kocha Arsene Wenger amesema kwamba, atafuatilia kwa karibu zaidi afya ya mchezaji huyo.