Saturday, March 10, 2012

Roberto Mancini amkasirisha Wenger

Kocha wa Arsenal Arsene Wenger amekasirishwa na kitendo cha Kocha wa Manchester City Roberto Mancini Kuongea hadharani kuelezea jinsi anavyomujhitaji Van Persie kwenye timu yake.

Gazeti la Uingereza London Evening Standard limesema kwamba Wenger amepatwa na hasira Kwa kitendo cha Mancini kumuongelea Mchezaji ambaye ana Mkataba na Timu mpaka mwaka 2013,Kwa sasa wenger Anapata wakati mgumu kuhakikisha Van Persie anaingia Mkataba mpya na Arsenal.

Van Persie Ameomba makubaliano juu Mkataba mpya yasogezwe mbele mpaka Mwisho wa msimu,Na inasemekana kumaliza Ndani ya nne bora kwenye ligi ya Uingereza ndicho kigezo kikubwa kitakachomfanya Van Persie Kubaki Arsenal.