Thursday, March 8, 2012

Gonzalo Higuain kuhamia Juventus


Higuain kwenda Juventus

Mshambuliaji wa Real Madrid Gonzalo Higuain anaweza kuhamia Juventus, habari kutoka kwa baba yake mzazi. Tovuti ya ESPN soccernet imeripoti.

Higuain ambaye ana miaka 24, amekuwa akihusishwa na kuondoka Bernabeu, ingawa mkataba wake sasa unaisha mwaka 2016, na Paris St Germain wamekiri kuwa watamuhitaji mchezaji huyo katika majira ya joto.

Hata hivyo JJuventus wamekuwa na mahusiano toka zamani na Jorge Higuain, babake Gonzalo na wakala wake., wamejihakikishia uwezekano wa kwenda Turin upo.

‘Ni faraja kuvutiwa na Juventus’ aliimbia Tuttosport. “Kwa sasa, Higuain anafikiria zaidi kuhusu Madrid, lakini mwezi mei tutaweza zungumza”

Juventus pia inasemekana wamevutiwa na kijana wa miaka 17 kutoka River Plate, Lucas Ocampos, ambae mkataba wake unaisha 2013

Wakala Pablo Martin Sabbag aliimbia Calcio Mercato: “naweza kukuhakikishia timu nyingi kutoka ulaya wanavutiowa nae”

Alipoulizwa kuhusu Juventus akaongeza, “Sipendelei kutaja majina, lakini naweza kusema timu tatu kutoka Italia zinamfuatilia”