Wednesday, March 7, 2012

Maafisa wa polisi wauwa Pakistan

Watu waliojihami kwa bunduki na maguruneti wamewauwa maafisa watatu wa polisi katika mji wa Peshawar Kaskazini Magharibi mwa Pakistan.

Watu watatu walishambulia kituo cha polisi katikati mwa mji huo na kisha kujilipua pale polisi walipoanza kuwakabili.
Ripoti zaidi zinasema polisi wengine wanne walijeruhiwa.

Wanamgambo wamekuwa wakiulenga mji wa Peshawar mara kwa mara katika miaka ya hivi karibuni.

Eneo hilo ni ngome ya wanamgambo walio na uhusiano na makundi ya Taliban na Al-Qaeda.