Monday, March 12, 2012

Van Persie akubali offer ya Man City?

Manchester City wako tayari kumfanya Robin Van Persie kuwa mchezaji anayelipwa mshara mkubwa kuliko mchezaji yoyote kwenye ligi kuu ya Uingereza, ambapo atakua akipokea kiasi cha paundi 210,000 kwa wiki.

Mkataba huo unathamani ya paundi milioni 10.9 kwa mwaka, Chazo kimoja cha The Sunday Times kimeripoti kwamba kimsingi Van Persie amekubali dili hilo litalomuingizia kitita kikubwa cha pesa.

Bado timu zote mbili za Manchester City na Arsenal hazijafanya makubaliano rasmi, Ingawa Arsenal inaonekana kutaka kumzuia mshambuliaji huyo nyota aliyepiga mabao 32 katika michezo 37 aliyocheza msimu huu asiondoke klabuni hapo.

Van Persie 28 anatarajia kumaliza mkataba wake na Arsenal mwisho wa msimu ujao (mwezi wa sita 2013) na kocha wa Manchester city amekua akielezea ni kwa kiasi gani anamkubali mshambulijai huyo.