Friday, March 9, 2012

Man City yavutiwa na Van Persie



Kocha wa Manchester City muitalia Roberto Mancini amekiri kuwa anatamani sana kumsajiri kinara wa kupachika mabao wa Arsenal mholanzi Robin Van Persie.

Kuna uvumi kuwa mpachika mabao huyo anaweza akaondoka msimu ujao hasa kutokana na hali ya Arsenal katika kufukuzia taji la Ligi kuu kuwa ndogo na ukame wa vikombe kwa zaidi ya miaka mitano sasa.

Hata hivyo sio rahisi Manchester City ikamchukua kirahisi kwani timu nyingi kubwa za Ulaya zitakuwa nyuma ya ununuzi huo tayari kuvunja akaunti zao mara tuu Arsenal itakapotangaza kumuuza.

Hata hivyo Mancini hana uhakika kama Van Persie ataondoka Arsenal

"Ni mchezaji mzuri sana, lakini nafikiri atabaki na Arsenal. Nafikiri kama kuna mchezaji mzuri atataka kuondoka kwenye klabu yake basi lazima tuvutiwe naye. Lakini kama mchezaji huyu atataka kubaki hatutakuwa na tatizo naye. Kwa maoni yangu, Van Persie atabaki Arsenal" alisema Mancini.