Thursday, March 8, 2012

Lucas Podolski ndani ya the Gunners


Arsenal Yakamilisha Uhamisho wa Lucas Podolski

Mshambuliaji wa Ujerumani Lucas Podolski atakua mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Arsenal wakati dirisha la usajili litakapofunguliwa baada ya Arsenal kukubaliana na Cologne(Klabu ya zamani ya Podolski) kwa kiasi cha paundi 10.9 milioni.

Hapo awali Cologne walikua wanahitaji kiasi cha paundi 18 milioni ambacho kilikataliwa na Arsenal ambao walikua tayari kutoa kiasi cha paundi 8 milioni.Arsenal walianza kufanya makubaliano binafsi na Podolski(26) kabla ya kuweka offer mpya iliyokubaliwa na Cologne.

Lucas Podolski mzaliwa wa Poland mwenye miaka 26 ameshafunga magoli 16 katika michezo 20 aliyochezea Cologne katika ligi ya Bundesliga(Ujerumani) msimu huu.

Lucas Podolski alisajiliwa na Cologne akitokea Bayern Munich mwaka 2009.Akiwa Bayern Munich Podolski hakufanikiwa kufanya vizuri hivyo kumfanya kukaa benchi kwenye mechi nyingi.Hata hivyo Podolski amekua na mafanikio mazuri kwenye timu ya Taifa ya Ujerumani akifanikiwa kufunga magoli 43 hivyo kumfanya kuwa mchezaji wa sita wa Ujerumani kuwahi kufunga magoli mengi kwenye ngazi ya taifa.