Friday, March 9, 2012

van Persie amtia hofu Wenger

TIMU ya Arsenal imeingia katika hofu kubwa kutokana na hali ilivyo kwa mchezaji wake tegemeo, Robin van Persie ambaye juzi alishindwa kufanya mazoezi na timu yake ya taifa ya Uholanzi, kwa kile kilichoelezwa kusumbuliwa na maumivu.

Mchezaji huyo alishindwa kucheza katika dakika zote pale Uholanzi ilipocheza na England, hivyo kuanza kuwatia hofu mashabiki wa timu hiyo.

Kocha Arsene Wenger amesema kwamba, atafuatilia kwa karibu zaidi afya ya mchezaji huyo.